Mtaarishaji na mwigizaji wa kike kutoka bongo movie nchini Mwanaher Afcely ametamba kuwa yupo vizuri kila idara,uku akidaiwa kufananishwa na nyota Riyama Ally
Mwanaher ametamba kuwa hajivunii kufanana na Riyama tu bali uwezo wake katika uigizaji na kufanya kwake vizuri ndio kunafanya mashabiki kushindwa kutofautisha utofauti wake na Riyama hasa kwa kuigiza kwa ufasaha
Mwanaher anafunguka kiafrika bila hofu kuwa "nipo kikazi zaidi na unajua kama nafananishwa na Riyama na anauwezo mkubwa lazima nijitaidi kufanya kazi kwa bidii ili nifanikiwe nakujituma zaidi ndio kitu kikubwa
Mwanadada huyu mwenye stashahada ya manunuzi amesema kuwa alikua anaigiza filamu kutoka kwa watu hadi alipotengeneza filamu yake ya pumu akiwashirikisha wakali wengine na kudai kuwa anahisi ana deni kubwa kufananishwa na Riyama


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni