Kurasa

Jumatano, 21 Septemba 2016

KALAMBATI LOBO YA JB KUONESHWA SIBUKA MAISHA IJUMAA KABLA YA KUINGIA SOKONI

Mcheza filamu maarufu Jacob stephen (JB) amefanya mkutano na waandishi wa habari kwa lengo la kutambulisha mfumo mpya wa kuonesha filamu kupitia media ya Sibuka Maisha channel 111 kwenye startimes kabla ya kuingia madukani.
Amesema filamu hiyo inaoneshwa kwa mara ya kwanza Ijumaa tarehe 23 mwezi huu saa 3 usiku na kurudiwa Jumamosi na Jumapili ili kuwapa muda mashabiki zake waweze kuona filamu hiyo
Aidha ameishukuru kampuni ya Steps entertainment kwa kuanzisha mfumo huu mpyaa wa kuonesha filamu kabla hazijaingia sokoni
Filamu hii inatarajia kuingia sokoni Jumatatu 26 mwezi wa 9 nchi nzima,kwa sasa hivi Jb anatamba sokoni na filamu ya chungu cha tatu akiwa na Wema Sepetu na wasanii wengine wengi.

Jumatano, 17 Februari 2016

MWANAHER YA MWANAHER YAKAMILIKA SOON ITAKUA MTAANI

 Baada ya kufanya vizuri kwenye filamu ya Pumu,mcheza filamu anaekuja juu kwa kasi Mwanaher amemaliza utengenezaji wa filamu ya Mwanaher aliyowashirikisha wa sanii nyota wa filamu nchini 



 Akifunguka kiafrika bila hofu yoyote amesema amepania kuteka soko la filamu nchini kwa kufanya kazi nzuri zenye viwango vikubwa sana amesema filamu hiyo amecheza na wasanii kama vile Stanley nsungu,Riyama Ally,Frola Mvungi na wengine wengi



MUONEKANO MPYA WA MUIGIZAJI CHUCHU ANSI





Jumanne, 16 Februari 2016

MWANAHER:NIPO VIZURI KILA IDARA

Mtaarishaji na mwigizaji wa kike kutoka bongo movie nchini Mwanaher Afcely ametamba kuwa yupo vizuri kila idara,uku akidaiwa kufananishwa na nyota Riyama Ally

Mwanaher ametamba kuwa hajivunii kufanana na Riyama tu bali uwezo wake katika uigizaji na kufanya kwake vizuri ndio kunafanya mashabiki kushindwa kutofautisha utofauti wake na Riyama hasa kwa kuigiza kwa ufasaha

Mwanaher anafunguka kiafrika bila hofu kuwa "nipo kikazi zaidi na unajua kama nafananishwa na Riyama na anauwezo mkubwa lazima nijitaidi kufanya kazi kwa bidii ili nifanikiwe nakujituma zaidi ndio kitu kikubwa
Mwanadada huyu mwenye stashahada ya manunuzi amesema kuwa alikua anaigiza filamu kutoka kwa watu hadi alipotengeneza filamu yake ya pumu akiwashirikisha wakali wengine na kudai kuwa anahisi ana deni kubwa kufananishwa na Riyama